Abstract
Je, amani ya kudumu inakuja nchini Sudan Kusini ? Hatimaye, rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wametia saini mkataba wa mwisho wa amani baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa jijini Khartoum nchini Sudan, ambao pamoja na mambo mengine, unasitisha vita na kuwezesha kuundwa kwa serikali ya pamoja, huku Machar akitarajiwa kurejea kama Makamu wa kwanza wa rais.